Swali: Ni ipi hukumu kwa wale wenye kuwatukana baadhi ya maimamu kwa mfano Imaam Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) na wanasema kuwa maneno yake ni ya kiakili na sio kutoka katika Qur-aan na Sunnah? Tunaomba utuwekee wazi uhakika wa maneno haya.

Jibu: Utumiaji wa akili haupingwi moja kwa moja kama wanavosema Ashaa´irah. Utumiaji wa akili haupingwi moja kwa moja kama jinsi hautegemewi peke yake. Inatumiwa pale ambapo itaenda sambamba na Shari´ah. Katika hali hii inatumiwa. Huu ndio mfumo wa Imaam Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah). Anatumia akili na kipimo pale inapoenda sambamba na Shari´ah. Anaitumia katika mipaka ya Shari´ah. Akili ni neema kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall). Hatuikanushi. Lakini akili haitumiwi peke yake. Ni lazima akili iwe inaafikiana na Shari´ah. Aliyesema maneno haya ni mjinga. Alosema haya ni mmoja katika watu wawili:

1 – Ima ni mpotevu – tunaomba kinga kwa Allaah. Anachotaka ni kuwapoteza waislamu kwa kuwatukania maimamu wao.

2 – Au ni mjinga. Anadai kuwa ni mwanachuoni na kwamba yeye ni msomi zaidi kuliko Abu Haniyfah. Hili ni tatizo. Baadhi yao wanadai kuwa ni wajuzi zaidi kuliko Abu Haniyfah, Maalik, Ahmad bin Hanbal na ash-Shaafi´iy. Baadhi yao wanadai hivi. Wanasema kuwa wao ni wanaume na sisi pia ni wanaume. Wao ni wanaume wanachuoni na wewe ni mwanaume mjinga:

قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ

“Sema: “Je, wanalingana sawa wale wanaouja na wale wasiojua?” Hakika wanakumbuka wenye akili tu”.” (39:09)

Maneno haya kuwasema vibaya wanachuoni ni khatari.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1431-08-08.MP3
  • Imechapishwa: 21/04/2015