Kufunga safari kuswali nyuma ya imamu mwenye sauti nzuri

Swali: Mtu anafunga safari kwa ajili ya kwenda kuswali nyuma ya imamu mwenye sauti nzuri au kwa ajili ya kufanya I´tikaaf kinyume na Misikiti mitatu.

Jibu: Ni mtu wa Bid´ah. Akifunga safari kwa ajili ya mtu mwenye sauti nzuri, huu ni uzushi. Kadhalika ni mtu wa Bid´ah ikiwa atafunga safari kwa ajili ya kufanya I´tikaaf kwenye Misikiti isiyokuwa Misikiti mitatu. Afanye I´tikaaf kwenye Msikiti wowote ulio karibu na yeye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1431-08-08.MP3
  • Imechapishwa: 21/04/2015