Wanachuoni juu ya mgonjwa mwenye kuomba kusomewa

Wanachuoni wameleta utatizi juu ya Hadiyth hii na kusema endapo mtu atalazimika kuomba mtu amsomee kwa kufikwa na kijicho, uchawi na jini anatoka miongoni mwa wale wenye kustahiki kuingia Peponi bila ya hesabu wala adhabu?

1 – Kuna wanachuoni waliosema kuwa huu ndio udhahiri wa Hadiyth. Anatakiwa kumtegemea Allaah na kuwa na subira na kuomba Allaah amponye.

2 – Wanachuoni wengine wakasema hili linahusu yule mtu aliyeomba kusomewa kabla ya kufikwa na ugonjwa. Kwa mfano akasema nisomee ili nisipatwe na kijicho, uchawi, jini, homa na kuchomeka. Huyu anakuwa ameomba kusomewa matabano kwa kitu anachokikhofia ambacho hakijatokea.

Wale wanaosomewa wengine wanatoka miongoni mwa watu hawa? Jibu ni hapana.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/552-553)
  • Imechapishwa: 24/07/2023