Wakati mwingine utasikia watu wakisema “Ibraahiym ni (خليل) wa Allaah, Muhammad ni mpenzi (حبيب) wa Allaah na Muusa ni msemezwa wa Allaah.” Wale wenye kusema kuwa Muhammad ni mpenzi wa Allaah, hili linatakiwa kuangaliwa vizuri. Kwa sababu mapenzi ya hali ya juu (خليل) yana daraja ya juu kuliko mapenzi ya kawaida (حبيب). Kwa hiyo kukisemwa ya kuwa Muhammad ni mpenzi wa Allaah, katika hili kuna aina fulani ya kushusha hadhi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu wapenzi wa Allaah ni wengi. Waumini pia wanapendwa na Allaah. Watenda wema wanapendwa na Allaah. Wenye kufanya uadilifu wanapendwa na Allaah. Wapenzi wa Allaah ni wengi. Lakini mapenzi ya hali ya juu hatujui kuwa yamethibiti isipokuwa kwa Muhammad na Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam). Kutokana na hili usawa ni kusema Ibraahiym ni (خليل) wa Allaah, Muhammad ni (خليل) wa Allaah na Muusa ni msemezwa wa Allaah.

Pamoja na kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisemezwa na Allaah maneno pasina ukatikati pindi alipopandishwa juu ya mbingu ya saba.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/554-555)
  • Imechapishwa: 24/07/2023