28. Kama unataka kuwa na afya

144 – ´Awn bin Ibraahiym amenihadithia: Ahmad bin Abiyl-Hawaariy amenihadithia: Nimemsikia baba yangu akisema: Nimemsikia Wahiyb bin al-Ward akisema:

”Aadam ameumbwa na mkate ukaumbwa pamoja naye. Chenye kuzidi juu ya mkate ni matamanio.”

Nikamuhadithia Sulaymaan bin Abiy Sulaymaan, ambaye akasema:

”Amesema kweli. Mkate na chumvi ni matamanio.”

145 – ´Awn bin Ibraahiym amenihadithia: Ahmad bin Abiyl-Hawaariy amenihadithia, kutoka kwa Abu Sulaymaan, aliyesema:

”´Umar amesema kuhusu maneno Yake Allaah (´Azza wa Jall):

إِنَّ الَّذِينَ يَغُضُّونَ أَصْوَاتَهُمْ عِندَ رَسُولِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ امْتَحَنَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ لِلتَّقْوَىٰ

”… hao ndio ambao Allaah amezisafisha nyoyo zao kwa ajili ya uchaji.”[1]

”Bi maana wameondosha matamanio yao kutokana nayo.”

146 – ´Awn amenihadithia: Ahmad ametuhadithia: Abu Sulaymaan ametuhadithia: Abu ´Aliy ´Abdus-Swamad al-Aswamm ametusimulia maneno mazuri pale aliposema:

”Wafungaji siku ya Qiyaamah watawekewa meza ya chakula. Watakula kutoka hapo na huku watu wako wanafanyiwa hesabu. Waseme: ”Ee Mola! Sisi tunafanyiwa hesabu na wale kule wanakula!” Ndipo aseme: ”Pindi mlipokuwa mnakula na kunywa, wao walifunga. Pindi mlipokuwa mmelala, wao walikuwa wamesimama kufanya ´ibaadah.”

147 – al-Husayn bin Hammaad adh-Dhwabbiy ametuhadithia: Qabiyswah bin ´Uqbah ametuhadithia, kutoka kwa al-Hasan bin Swaalih, kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin Rufay´, aliyesema kuhusu:

كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا أَسْلَفْتُمْ فِي الْأَيَّامِ الْخَالِيَةِ

“Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyoyatanguliza katika siku nyingi zilopita!”[2]

”Kwa sababu ya kufunga.”

148 – Salamah bin Shabiyb amenihadithia: Sahl bin ´Aaswim ametuhadithia, kutoka kwa Silm bin Maymuun al-Khawwaasw: Nimemsikia ´Abdul-´Aziyz bin Muslim akisema: Nimemsikia Sufyaan ath-Thawriy akisema:

”Kula utakavyo na usinywe. Usipokunywa basi hutojiwa na usingizi.”

149 – ´Awn bin Ibraahiym amenihadithia: Ahmad bin Abiyl-Hawaariy amenihadithia: Nimemsikia Abu Sulaymaan akisema:

”Kutoka tumboni kwenda mpaka kwenye macho kuna mishipa miwili; tumbo linapokuwa nzito basi macho yanafungika na tumbo linapokuwa jepesi macho yanafunguka.”

150 – Muhammad bin Idriys amenihadithia: ´Amr bin Aslam ametuhadithia, kutoka kwa Silm bin Maymuun al-Khawwaasw: ´Uthmaan bin Zaa-idah amenihadithia:

”Sufyaan ath-Thawriy aliniandikia: ”Ikiwa unataka mwili wako kuwa na afya na ulale kidogo, basi kula kidogo.”

[1] 49:3

[2] 69:24

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 98-100
  • Imechapishwa: 24/07/2023