Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

وعن أنس رضي الله عنه قَالَ : مَرَّ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم بامرأةٍ تَبكي عِنْدَ قَبْرٍ، فَقَالَ: (اتّقِي الله واصْبِري) فَقَالَتْ : إِليْكَ عَنِّي؛ فإِنَّكَ لم تُصَبْ بمُصِيبَتي وَلَمْ تَعرِفْهُ، فَقيلَ لَهَا : إنَّه النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم فَأَتَتْ بَابَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم، فَلَمْ تَجِدْ عِنْدَهُ بَوَّابينَ، فقالتْ : لَمْ أعْرِفكَ، فَقَالَ: (إنَّمَا الصَّبْرُ عِنْدَ الصَّدْمَةِ الأُولى). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

.وفي رواية لمسلم: (تبكي عَلَى صَبيٍّ لَهَا)

31 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpitia mwanamke ambaye alikuwa analia kwenye kaburi na kumwambia: “Mche Allaah na kuwa na subira!” Akasema: “Niondokee, hujafikwa na msiba ulonifika!” [na mwanamke huyo] hakumtambua [aliyemwambia vile].  Akaambiwa: “Huyo alikuwa ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akaenda mpaka kwenye mlango wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hakukua walinzi. Akamwambia: “Sikukutambua.” Akasema: “Hakika mambo yalivyo subira wakati wake ni pale mwanzoni mwa kupatwa na msiba.”[1]

Miongoni mwa faida ya Hadiyth hii ni pamoja na kwamba haifai kwa mtu ambaye ni msimamizi wa mambo ya waislamu akaweka walinzi wenye kuwazuia watu ikiwa watu wanamuhitaji. Isipokuwa tu ikiwa mtu anakhofia watu wakawa wengi na kujaa na kumshughulisha kwa kitu ambacho wanaweza kufanyiwa hata wakati mwingine, katika hali hii ni sawa.

Ubishaji hodi haukuwekwa [katika Shari´ah] isipokuwa ni kwa sababu ya kuangalia kwanza ni nani mbishaji na kwa sababu mtu aweze kumwingiza nyumbani kwake yule anayemtaka na kumzuia yule asiyemtaka.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/228-229)
  • Imechapishwa: 23/02/2023