Swali: Sisi huku kwetu kuna kundi la Suufiyyah waabudu makaburi ambao wanafanya Shirki, Bid´ah na ukhurafi. Tunapotaka kuwalingania katika Tawhiyd na Sunnah wanakwepa vikao vyetu kwa sababu sisi ni Wahhaabiyyah. Hata hivyo wanakuja sehemu za kutoa pole. Je, inajuzu kwetu kuwalingania watu hawa katika Tawhiyd na Sunnah sehemu kama hizi?

Jibu: Nendeni nao kwa upole na ulaini pengine Allaah Akawaongoza. Wavuteni. Msiwashambulie na kuwaita kuwa ni makafiri na washirikina. Nendeni nao pole pole kwa utulivu, hekima na ulaini pengine Allaah Akawaongoza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (04) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir–14331228.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015