Swali: Baadhi yao wamesema ya kwamba kila ambacho kimewezekana kuwa ni miujiza kwa Nabii kinawezekana vilevile kuwa ni karama kwa walii hata kuhuisha maiti. Wamenasibisha hilo kwa Salaf. Je, ni sahihi?

Jibu: Kuhuisha maiti hili ni batili. Hakuna yeyote katika mawalii mwenye kuhuisha maiti. Hii ni miujiza kwa ´Iysaa (´alayhis-Salaam) peke yake. Haiwi kwa mwengine. Ama karama za mawalii ni miujiza ya Manabii kwa kuwa hawakufikia karama hizi isipokuwa kwa sababu ya kuwafuata kwao Manabii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-2-8.mp3
  • Imechapishwa: 18/08/2020