al-Fawzaan kuhusu majaaz katika Qur-aan

Swali: Je, katika Qur-aan kuna kitu katika majaaz?

Jibu: Hapana. Qur-aan yote ni hakika na ndani yake hakuna majaaz. Wale wanaosema kuna majaaz katika Qur-aan wamekosea katika hili. Ibn-ul-Qayyim amewaita kuwa ni “Twaaghuut wa Majaaz”. Wakija kwenye majina na sifa za Allaah ndio wanasema kuwa ni majaaz. Wanahukumu kwa kutumia Twaaghuut ambayo ni majaaz. Haijuzu kufanya hivi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-2-8.mp3
  • Imechapishwa: 18/08/2020