Swali: Mwenye kuwasifu watu wa Bid´ah na kuwatakasa anaambiwa kuwa ni mtu wa Bid´ah?

Jibu: Ikiwa kweli ni watu wa Bid´ah… kwa sababu tatizo ni kuwa wanaita kila kitu kuwa ni Bid´ah. Vijana wenye hamasa na ghera kila kitu kwa mujibu wao ni Bid´ah. Bid´ah ina vidhibiti vyake na dalili katika Shari´ah. Hakuna anayehukumu kuwa kitu fulani ni Bid´ah isipokuwa wanachuoni.

Ikithibiti kuwa kitu hichi ni Bid´ah mtu ajiepushe nacho na ajiepushe na yule mwenye kukifanya au kulingania kwacho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-2-8.mp3
  • Imechapishwa: 18/08/2020