Mwenye kufasiri Qur-aan kwa kutumia akili zake

Swali: Ni yapi maoni yako kwa mwenye kufasiri Qur-aan bila ya elimu na anaponasihiwa anasema “Allaah ametujaalia akili”?

Jibu: Haijuzu kufanya hivi. Huku ni kuzungumza juu ya Allaah pasina elimu. Imekuja katika Hadiyth:

“Mwenye kusema juu ya Qur-aan kwa maoni yake na kwa yale asiyoyajua, ajiandalie mahala pake Motoni. Amekosea hata kama atapatia.”

Haya yamesemwa na Haafidhw Ibn Kathiyr mwanzoni wa Tafsiyr yake na ameifanya isnadi yake kuwa Hasan. Huku ni kuzungumza juu ya Allaah pasina elimu. Wewe unafasiri Maneno ya Allaah kwa akili yako? Maneno ya Allaah hayafasiri isipokuwa kwa njia za Tafsiyr zinazokubalika: kufasiri Qur-aan kwa Qur-aan, Qur-aan kwa Sunnah, Qur-aan kwa maneno ya Taabi´uun au kufasiri Qur-aan kwa lugha ya kiarabu ambayo imeteremka kwayo. Ama akili haina nafasi katika kufasiri Qur-aan.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-2-8.mp3
  • Imechapishwa: 18/08/2020