Swali: Anauliza hukumu ya mwanamke kutoka kwenda kufanya Da´wah kama wanavyofanya baadhi ya wanaume wa [Jamaa´at] at-Tabliygh wanapotoka wakifuatana na wake zao pamoja nao. Je, hili linajuzu au hapana?

Jibu: Hii kwa uhakika ni Bid´ah nyingine ambayo tulikuwa hatujaisikia hapo kabla. Na nilikuwa nalisema tangu miaka, wakati walipozusha baadhi ya watu kuwaita baadhi ya wasichana waliohitimu katika baadhi ya masomo ya Kishari´ah, wanawaita “Daa´iyaat” (Madu´aat wakike). Tulikuwa – Subhaana Allaah. Tokea lini katika Uislamu kulikuwa Daa´iyaat? Alikuwa mama wa waumini ´Aa´ishah (Radhiya Allaahu ´anha) ni bingwa wa Fiqh na elimu kwa kiasi ambacho aliwazidi kwa hilo wengi katika Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na kwa ajili hiyo, walikuwa [Maswahabah] wakijua fadhilahzake, ubora wake katika uwanja huu, kwa kuwa yeye alikuwa kwanza ni mke bikira wa Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam). Isitoshe alikuwa ni katika mke anayempenda zaidi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kushahidilia kwake yeye mwenyewe. Pamoja na hivyo, alikuwa hasafiri kwa ajili ya kufanya Da´wah na wala kutoka khuruuj hizi.

Ambapo si mbali sana, mimi nimetoa mfano kwa kuashiria, na uashirio unatosheleza kwa mtu mwenye busara. Kwa kuwa kutoka makundi namna hii na hakuna ndani yake isipokuwa mwanachuoni mmoja au hakuna hata huyo mmoja, na hao wengine hawana elimu. Sisi tunawanasihi na tutaendelea kufanya hivyo, kama tulivyofungua kikao chetu hichi na vikao vingine kwa mfano wa kauli yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambayo nimetangulia kuisema:

“Kundi la watu halikusanyiki katika moja ya Nyumba (Msikiti wa) Allaah, wakisoma Kitabu cha Allaah na wakakidurusu baina yao, ila huteremka juu yao utulivu, Malaika huwazunguka, rehema huwaenea, na Allaah huwakumbuka kwa wale walioko pamoja naye.”

Tunawanasihi hivi daima na kila siku. Badala ya khuruuj hizi ambazo hawakufanya Salaf tokea karne kumi na nne. Sisemi kwamba hawana Salaf, kiuna Salaf wanaomithili karne tatu tu, katika karne zote hizi za Kiislamu hatujaona ya kuwa kunamwanachuoni anatoka na akiwa na watu kumi, ishirini, thalathini au zaidi kwa ajili ya kufikisha Da´wah. Ufikishaji wa Da´wah unahitajika kwa wanachuoni na sio kwa ´Awwaam. Nilikuwa nawanasihi watu hawa washikamane na Nyumba miongoni mwa Nyumba za Allaah, wakisome Kitabu cha Allaah na wakidurusu baina yao mpaka apatikane kwao mwanachuoni ambaye atasimama mbele ya watu, hafanyi makosa katika kusoma Aayah ya Allaah wala Hadiyth ya Mtume. Lakini hili [yaani makosa haya] kwa masikitiko makubwa, tunayasikia mara nyingi sana kabisa. Tulikuwa tunawanasihi watulizane katika Nyumba ya Allaah na wajifunze, na leo ghafla tunaona, kama mfano wa msemo wa ´Awwaam usemao:

“Tulikuwa chini ya mvua, na hivi tuko chini ya miwani ya darubini”.

Tulikuwa tunalalamika khuruuj zinazofanywa na wasiokuwa katika wanachuoni katika wanaume, na leo ghafla tunaona ya kwamba maradhi haya yamewaendea hata wanawake. Hivi kweli hawajui watu hawa ya kwamba Allaah (´Azza wa Jalla) kwanza Kateremsha Aayah ndani ya Qur-aan iliyo wazi. Akasema (Ta´ala) Akiwaambia wanawake wa Ummah kupitia wake za Mtume wa Ummah:

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ

“Na bakieni majumbani mwenu na wala msijishaue kuonyesha mapambo kama walivyokuwa wakijishaua kuonyesha mapambo yao wanawake wa kipindi cha kikafiri hapo mwanzoni.” (33:33)

Maana ya “bakieni” ni “tulizaneni”, yaani “bakieni” msitoke katika manyumba yenu. Na ikiwa mtatoka katika manyumba yenu kwa haja basi ni lazima kwenu [kuzingatia masharti yafuatayo, miongoni mwayo]

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ

“Na bakieni majumbani mwenu na wala msijishaue kuonyesha mapambo kama walivyokuwa wakijishaua kuonyesha mapambo yao wanawake wa kipindi cha kikafiri hapo mwanzoni.” (33:33)

Je, hivi kweli watu hawa hawajui kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba ni bora kwa mwanamke kutotoka kwenda kuswali Jamaa´ah na Waislamu, wakati Mtume wa Mola wa walimwengu alisema:

“Na manyumba yao ni bora kwao.”

Bali kasema ´Aa´ishah (Radhiya Allaahu ´anhaa):

“Lau angelijua Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) waliyozua wanawake baada yake basi angeliwakataza kwenda Misikitini.”

Mtume (´alayhis-Salaam) kaja kwa Uislamu wa kati na kati:

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا

“Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah wa kati na kati.” (02:143)

Uislamu usiokuwa ndani yake na kukazia sana na wala kuchuja, usiokuwa na uchupaji wa mipaka wala uvunjaji, bali ni kama Alivyosema:

وَكَانَ بَيْنَ ذَٰلِكَ قَوَامًا

“Wanakuwa wakati na kati baina ya hayo.” (25:67)

Hakukuharamishwa kwa wanawake kushirikiana na Waislamu kuswali Misikitini, lakini alisema:

“Na manyumba yao ni bora kwao.”

Hakuwaharamishia. Kwa kuwa mwanamke anaweza kuhitajia wakati mwingine kuswali Msikitini ili asikilize mawaidha, ajifunze elimu na khaswa katika zama kama hizi ambapo waalimu na wasomaji wamekuwa wachache mno. Tunachotaka kusema ni kuwa, kakataza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye Allaah Kamteremshia na Kuwaambia wake zake kwa Kauli Yake:

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ

“Bakieni majumbani mwenu.” (33:33)

Wanawake wasiokuwa wa Mtume (´alayhis-Salaam) ni wenye haja zaidi ya mfano wa ujumbe kama huu. Hali kadhalika kapendelea kwa wanawake washikamane na kuswali faradhi zao tano kwa siku majumbani mwao. Akasema:

“Na manyumba yao ni bora.”

Vipi basi watu hawa ikiwa kweli wanajua Sunnah, na ikiwa hawajui hili ni jambo la uchungu, na ikiwa wanajua kisha wakaenda kinyume chake hili ni chungu zaidi. Hawakutosheka na khutuba ya watu hawa ambao wao husema daima ya kwamba kutengemaa na kuokoka kwa Ummah huu ni kwa kufuata Sunnah ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vipi basi watakwenda kinyume na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika makumi ya mambo ya msingi wanayoyafanya, miongoni mwayo ni kalima hii ambayo tumeifanya darsa. Kuokoka kwetu na kutengemaa kwetu ni kwa kufuata Sunnah ya Mtume wetu. Mtume wetu alikuwa hasemi maneno haya, alikuwa anasema:

“Amma ba´ad, kwa hakika bora ya maneno ni Maneno ya Allaah, na uongofu bora ni uongofu wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Ikiwa hawajui, basi hii ni shari. Na ikiwa wanajua, basi hii ni shari zaidi. Na mimi nasema wanajua. Mimi naogopa ya kwamba hawafanyi hivyo kwa jengine, isipokuwa ni kwa kuwa hawako pamoja na Ahl-us-Sunnah katika kauli ya Mtume wa Sunnah:

“Kwa hakika kila Bid´ah ni upotofu, na kila upotofu ni Motoni.”

Bali kinyume chake, Da´wah yao imejengeka juu ya kukosekana athari ya Sunnah hii na hivyo kwa Bid´ah hii. Kwa sasa tunaona kwa ghafla wamejitokea wanawake pia wakitoka na wanaume.

Ametakasika Mola Wangu. Bora ya watu ni Maswahabah wa Mtume (´alayhis-Salaam), wao ndio watu viongozi wa walimwengu, tukianzia kwa Abu Haniyfah na Imaam Ahl-us-Sunnah, je walikuwa wanawake wa wanachuoni hawa wa maimamu hawa wakitoka pamoja na wake zao katika njia ya kufanya Da´wah? Hapana, tena hapana, tena hapana! Vipi basi wanafanya watu hawa? Hili linatilia nguvu ya kwamba watu hawa wanakwenda kinyume na kauli zao kwa vitendo vyao. [Wanasema]:

“Mafanikio ni kwa kufuata Sunnah ya Mtume wa Allaah”

Kisha wao ndio wa kwanza kwenda kinyume na hilo? Na bado, wanayoyafanya sio katika ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Je, wameitekeleza kihakika na kufuata Sunnah ya Mtume (´alayhis-Salaam)? Huo ni ukumbusho, na ukumbusho unamfaa muumini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (686)
  • Imechapishwa: 03/09/2020