Swali: Nina ndugu ambaye amesafiri kwenda kwenye kijiji nje ya mji huu. Akafika kwenye misikiti mitatu ili kuswali swalah ya ijumaa, lakini kila msikiti akakuta una kaburi. Hivyo akawa anaswali Dhuhr nyumbani. Je, ni sahihi?

Jibu: Ni sawa ikiwa kama makaburi yako ndani ya misikiti. Usiswali kwenye msikiti uliojengwa juu ya kaburi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuswali makaburini na kufanya makaburi ni mahala pa kuswalia. Makatazo yanaonyesha kutosihi. Umefanya sawa. Badala yake swali Dhuhr. Ama ikiwa kaburi limetengana na msikiti na liko nje ya msikiti, halidhuru swalah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (30) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2025-12-1435.mp3
  • Imechapishwa: 16/06/2015