Lililo na usalama au lepesi?

Swali: Ni kipi kinachopewa kipaumbele katika Shari´ah; kilicho na usalama au chepesi?

Jibu: Kilicho na usalama inapokuhusiana na utatizi.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katu hakuwa na uwezo wa kufanya mambo mawili isipokuwa anafanya lile ambalo ni lepesi zaidi. Hili linahusiana na pale ambapo yote mawili yamo katika Shari´ah. Katika hali hii mtu anafuata lile ambalo ni lepesi. Mfano wa hili ni swalah katika safari. Inajuzu kuswali Rakaa kamilifu, na ndio asli, lakini hata hivyo kufupisha [swalah] ndio bora zaidi kwa sababu ni Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika safari. Katika hali hii ni bora zaidi kuchukua njia sahali kuliko kutendea kazi asli.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20-%201%20-%202%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015