Mtu anapata kitu kilichobana kwenye mguu baada ya swalah

Swali: Nilitawadha kwa ajili ya Maghrib na nikaswali. Kisha baada ya swalah nikaona kuna kitu kilikuwa kimekamata kwenye mguu wangu na nikawa nimekiondosha. Ni ipi hukumu ya wudhuu´ na swalah yangu?

Jibu: Ikiwa kitu hicho kilikuwa kimebana ina maana ya kwamba maji hayakufika kwenye ngozi chini yake. Kiondoshe, utawadhe na urudi kuswali tena. Ni wazi ya kwamba kuna sehemu katika kiungo chako cha mwili ambayo haikupatwa na maji. Hii ni yakini. Kilicho bana kiko wazi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20-%201%20-%202%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015