Swali: Je, wasiwasi ni maradhi kwa njia ya kwamba mwenye wasiwasi akitumbukia katika kupetuka mipaka au kuchuja Sunnah anapewa udhuru?

Jibu: Hapana. Hapewi udhuru. Ameamrishwa kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Dini iko wazi hakuna maze. Ni kwa nini asitilii umuhimu wa kujifunza Sunnah na yale waliyofuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake na yeye akayafuata?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20-%201%20-%202%20-%201436.mp3