Wakati ambapo mnaposikia sauti ya kawaida kutoka msikitini

Swali: Kuna watu ambao nyumba au kazini kwako kuko mbali na msikiti kwa mita 500 na wanasikia adhaana. Je, wanalazimika kuhudhuria msikitini?

Jibu: Ikiwa wanasikia adhaana wanalazimika. Hapa tunazungumzia pale ambapo ni sauti ya kawaida na sio kupitia kipaza sauti. Pale ambapo wanasikia adhaana ya kawaida. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayesikia adhaana na asiitikie basi hana swalah isipokuwa akiwa na udhuru.”[1]

Akaulizwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa): “Ni udhuru upi?” Akasema: “Khofu au maradhi.”

Ni lazima kwao kujitahidi kuweza kuswali na ndugu zao.

Sauti kupitia kipaza sauti inasikiwa kwa mbali. Kinachozingatiwa ni ile sauti ya kawaida wakati ambapo hakuna fujo na upepo umetulia. Katika hali hiyo inatosha ikiwa wanasikia.

Swali: Hiyo maana yake ni kwamba haiwalazimu watu wengi kwa sababu pengine sauti ya kawaida…

Jibu: Kinachozingatiwa ni sauti ya kawaida. Sauti ya kipaza sauti inafika mbali.

Swali: Kuna watu wengine ambao maeneo walipo kuko mbali na msikiti kwa mita 200 na hawasikii adhaana. Je, wanalazimika kuhudhuria swalah ya mkusanyiko?

Jibu: Wanatakiwa kwenda msikitini ikiwa sauti ya muadhini sio nyonge au wako katika majengo ambayo yanazuia sauti ya adhaana. Kwa sababu mita 200 ni karibu. Sauti inafika mbali zaidi ya hivo. Baadhi ya watu wanaishi maeneo ambapo kuna majengo marefu yanayozuia kufikiwa na sauti. Kwa hivyo wanapaswa kwenda ikiwa wanatambua kuwa endapo ingelikuwa sio vizuizi hivi basi wangelisikia sauti. Jengine ni kwamba muumini anatakiwa kuhifadhi swalah ya mkusanyiko hata kama msikiti utakuwa mbali, kwa sababu anataraji yaliyoko kwa Allaah hata kama atakuwa ndani ya gari. Kuna faida kubwa.

[1] Ibn Maajah (785).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23109/حكم-الجماعة-لمن-يسمع-الاذان-العادي-والمكبر
  • Imechapishwa: 05/11/2023