70. Aliandika barua ngapi Mtume aliwatumia wafalme?

Swali 70: Aliandika barua ngapi kuwatumia wafalme?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituma barua kwenda kwa:

1 – Hiraqli wa Rumi.

2 – Kisraa.

3 – an-Najaashiy. Udhahiri ni kwamba hakuwa akiitwa Aswhamah.

4 – Muqawqis wa Misri.

5 – Mundhir bin Saawaa.

6 – Jayfar bin al-Julandiy na ´Abd bin al-Julandiy wa Oman.

7 – Huudhah bin ´Aliy wa Yamaamah.

8 – al-Haarith bin Abiys-Shamr al-Ghassaaniy wa Shaam.

9 – Musaylimah.

Wafalme wote hawa na wajumbe wake wamekwishatangulia, isipokuwa barua yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenda kwa Musaylamah. Barua yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kwenda kwa Musaylamah aliituma kupitia mjumbe wake Musaylimah mwenyewe ambaye alikuja nayo kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Barua yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilikuwa ni jibu la baru yake.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 142
  • Imechapishwa: 05/11/2023