116. Makatazo ya kusimama kwa ajili ya mtu aliyekaa chini

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Katika Hadiyth hii (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewakataza kuacha kusimama licha ya kuwa ni faradhi kusimama kwa ajili ya kuswali. Ametoa sababu kwamba waswaliji kuswali kwa kusimama nyuma ya imamu aliyeketi chini ni jambo linafanana na matendo ya wafursi na warumi kwa wakuu wao. Ni jambo linalotambulika kuwa imamu yule anayeswalisha amenuia kumsimamia Allaah na si yule imamu wake. Huku ni kutilia mkazo wa kusimama kwa ajili ya mtu aliyeketi chini. Amelikataza hilo pia kwa sababu ya kujifananisha ingawa mtu hakukusudia hivo. Kwa ajili hiyo amekataza kumsujudia Allaah kwa kumwelekea mtu au kwa kukielekea kitu kinachoabudiwa badala ya Allaah, kama vile moto na mfano wake. Hadiyth hii vilevile inakataza matendo yanayofanana na matendo ya wafursi na warumi ijapo nia zetu zinatofautiana na nia zao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: ”Msifanye hivo.” Nini kingine kinachohitajika kusemwa linapokuja suala la makatazo ya kujifananisha nao kidhahiri?

Isitoshe Hadiyth hii kuhusu kukaa kwa imamu ni mamoja ikiwa bado inafanya kazi au imeshafutwa, bado hoja yake ni yenye kusimama. Kwa sababu ufutwaji wa kukaa chini hakuonyeshi kuharibika kwa sababu hiyo. Hakika mambo yalivyo ni kuwa inapelekea lipo jambo jingine lenye nguvu zaidi, kama vile jambo la kusimama ndani ya swalah ni faradhi ndani ya swalah. Faradhi haidondoki kwa sababu tu ya kule kujifananisha kwa nje. Suala hili ni jambo la ijtihaad. Ikiwa kujifananisha kwa nje hakudondoshi jambo la faradhi, basi sababu hiyo ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haiwezi kupingwa wala kufutwa. Kwa sababu kusimama ndani ya swalah sio jambo la kujifananisha katika uhalisia na hivyo haliwi lenye kukatazwa. Hukumu ikitolewa sababu kisha baadaye hukumu hiyo ikafutwa pamoja na kubaki kwa sababu hiyo, basi ni lazima kuwepo jambo jingine lenye nguvu zaidi kuliko sababu hiyo wakati wa kufutwa kwake au udhaifu wa athari yake. Hata hivyo haiwezekani ikawa sababu yenyewe ndio batili. Haya yote ni pale ambapo hukumu inakuwa yenye kufutwa. Kusemwe nini ikiwa Hadiyth hii bado ni yenye kufanya kazi na wapo Maswahabah wengi walioitendea kazi baada ya kufariki kwake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Pamoja na kwamba walikuwa wanajua namna alivyoswali wakati alipokuwa mgonjwa. Amri yake imepokelewa kwa mapokezi mengi ambayo ni Swahiyh na yaliyo wazi, kwa ajili hiyo haiwezekani Hadiyth kuhusu ugonjwa ikawa imeifuta, jambo ambalo limethibitishwa maeneo mengine. Kwa hivyo Hadiyth bado inafanya kazi, ima kwa sababu yote mawili yanawezekana – hali ya kusimama haipingani na hali ya kukaa chini – au inapokuja kutofautisha kati ya ambaye anaanza kuswali hali ya kuwa ameketi chini au ambaye ameanza kuswali hali ya kuwa amesimama, kwa sababu swalah hiyo haingii ndani ya ”na akiswali kwa kukaa chini” na kutokuwepo madhara ya sababu iliyotolewa. Aidha bora ni kujenga ile sehemu ya mwisho ya swalah juu ya ile sehemu yake ya mwanzo kuliko kuijenga juu ya swalah ya imamu.”[1]

[1] Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiym, uk. 32

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 173-174
  • Imechapishwa: 05/11/2023