Josho la janaba kwa wanawake waliosuka nywele

Swali: Tunaomba utukhabarishe namna ya kuoga josho la janaba kwa sababu baadhi ya wanawake wanaosha sehemu ya mwisho ya nywele na wanasema kuwa inafaa na kwamba kufanya hivo kunamtosha na kuosha kichwa kizima. Wakati mwingine wanaosha sehemu ya kichwa kwa njia ya kulowesha ile sehemu ya mwisho ya nywele na baadhi yake. Je, inafaa? Au wanatakiwa kuosha nywele kichwa kizima ni mamoja nywele hizo zimesukwa au hazikusukwa?

Jibu: Sunnah ni mtu mosi kutamba kwa maji baada ya jimaa, kisha atawadhe wudhuu´ wa swalah halafu ajimiminie maji juu ya kichwa chake mara tatu, kisha aoshe sehemu iliobaki ya mwili wake kwa kuanza na upande wake  wa kulia kabla ya upande wa kushoto mpaka atakapomaliza kuoga.

Inamtosha mwanamke akijimiminia maji juu ya kichwa mara tatu. Umm Salamah amesema:

“Ee Mtume wa Allaah! Mimi ni mwanamke ninayefunga nywele za kichwani mwangu. Nizifungue wakati wa kuoga janaba?” Akasema: “Inakutosha kumwaga juu ya kichwa chako konzi tatu halafu maji yatakuenea.”

Ukizimiminia konzi tatu za maji na yakazienea basi huna haja ya kuzifungua. Vivyo hivyo kuhusu mwanaume ikiwa yuko na nywele nyingi atazimiminia maji na wala hahitaji kuzifungua.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23110/ما-كيفية-الغسل-من-الجنابة-للنساء
  • Imechapishwa: 05/11/2023