Swali: Nimepewa mtihani wa watoto wa ami yangu wasioswali. Je, inafaa kwangu kuwasalimia au kula nao?

Jibu: Muda wa kuwa hawaswali na swalah ni nguzo miongoni mwa nguzo za Uislamu… isitoshe Allaah (Ta´ala) amesema:

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ

“Hutopata watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake.” (58:22)

Kuna kupinga kupi kukubwa kuliko kutangaza kwa mtu kuacha swalah? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Baina ya mtu na kufuru au shirki ni kuacha swalah.”

´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Hana funga katika Uislamu kwa mwenye kuacha swalah.”

Allaah (Ta´ala) amesema katika Suurah al-Mudaththir:

مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ

“[Watawauliza]: “Nini kilichokuingizeni katika [Moto wa] Saqar?” Watasema: “Hatukuwa miongoni mwa wanaoswali.” (74:42-43)

Wasuse.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Khaatam-ul-Mursaliyn https://godian.af.org.sa/sites/default/files/2017-10/lqa-mftoh-godian.mp3
  • Imechapishwa: 17/10/2022