Kupeana kiapo kati ya watu wawili kuacha maasi

Swali: Amekula kiapo (البيعة) ya kuacha mambo ya haramu. Je, inasihi kufanya hivo kwa asiyekuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Ndio. Kitendo cha wao kutomuasi Allaah ni jambo zuri.

Swali: Nakusudia endapo watu wawili watawekeana kiapo cha kuacha maasi.

Jibu: Hapana. Jambo hilo linakuwa kwa mtawala. Jambo la kula kiapo linakuwa kwa mtawala.

Swali: Nakusudia wakipeana kiapo kati yao cha kuacha maasi?

Jibu: Hapana, hakuna haja ya kupeana kiapo. Ni lazima kwao kupeana wasia na kunasihiana na kutubu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22015/هل-تصح-البيعة-بين-الناس-لترك-المعاصي
  • Imechapishwa: 16/10/2022