Swali: Baadhi ya watu wanajiua kutokana na sababu fulani na fulani. Je, mtu huyu atafanyiwa hesabu siku ya Qiyaamah?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kuiua nafsi yake kwa kitu basi ataadhibiwa kwacho siku ya Qiyaamah.”

Haijuzu kwa mtu kujiua kwa sababu ya kitu fulani na fulani au kwa ajili ya kumtetea fulani. Amtetee lakini asijiue nafsi yake.

Swali: Je, mtu huyu atafanyiwa hesabu?

Jibu: Hesabu yake iko kwa Allaah. Yeye ndiye atamfanyia hesabu. Akitaka kumsamehe basi atamsamehe na akitaka kumuadhibu basi atamuadhibu. Jambo liko mikononi Mwake (Subhaanahu wa Ta´ala). Yeye anamuadhibu na kumrehemu amtakaye. Hapa ni kwa yale madhambi yaliyo chini ya shirki.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22014/ما-جزاء-من-يقتل-نفسه
  • Imechapishwa: 16/10/2022