Swali: Aws bin Aws ath-Thaqafiy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Atakayejitwaharisha na kuoga siku ya ijumaa, akaenda kwa muda na mapema, akatembea na asipande, akawa karibu na imamu, akasikiliza na asifanye upuuzi, basi hulipwa kwa kila hatua moja ujira wa swawm ya mwaka mzima na kisimamo chake cha usiku.”[1]

Jibu: Hadiyth hii haina neno. Ni Hadiyth inayozungumzia siku ya ijumaa.

Swali: Ni wakati gani kwa kuzingatia nyakati za leo?

Jibu: Ni kwenda mapema ijumaa.

Swali: Ni saa ngapi kwa njia ya makisio?

Jibu: Allaah ndiye anajua zaidi. Baada ya kuchomoza jua na baada ya kula chakula cha asubuhi na akamaliza haja zake ajielekeze.

[1] Swahiyhh kwa mujibu wa Shaykh al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/433)”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22002/متى-يبدا-فضل-التبكير-للصلاة-يوم-الجمعة
  • Imechapishwa: 17/10/2022