23. al-Awzaa´iy akihimiza Sunnah na akitahadharisha Bid´ah

3 – Miongoni mwa maneno ya wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahabah amesema al-Awzaa´iy ´Abdur-Rahmaan bin ´Amr ambaye amekufa mwaka wa 157:

“Lazimiana na Aathaar za waliotangulia… “

Lazimiana na njia ya Maswahabah na wale waliowafata kwa wema kwa sababu wamejengeka juu ya Qur-aan na Sunnah.

“… hata kama watu watakukataa… “

Bi maana watakutenga na kujiweka mbali nawe.

“… na jihadhari na maoni ya watu… “

Tahadhari na maoni ya watu. Nayo ni yale yaliyosemwa kwa maoni tu pasi na kutegemea Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

“… hata kama watakupambia kwa maneno.”

Watakupambia na kuyafanya vizuri matamshi. Batili haigeuki kuwa haki kwa kupambwa na kufanywa nzuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 43-44
  • Imechapishwa: 17/10/2022