Swali: Jumatatu iliyopita wakati ambapo nilikuwa natufu kwenye Ka´bah pembezoni mwangu kulikuwepo kundi la watu katika du´aa yao wanaomba msaada asiyekuwa Allaah na wakifanya hivo kwa sauti ya juu. Katika hali kama hii ni lipi la wajibu ninalotakiwa kufanya?
Jibu: La wajibu kwako kufanya ni kuwanasihi na kuwaambia kuwa haijuzu, wamche Allaah na ni shirki. Waambie kuwa hii ni shirki kubwa. Waambie wamche Allaah. Wakipokea nasaha yako, himdi zote ni za Allaah, na wakikataa wewe utakuwa umetekeleza wajibu wako. Lakini usitumie ukali na hilo likapelekea kutopokea nasaha zako. Tumia nasaha na uwawekee wazi.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_fitan-14-08-1433.mp3
- Imechapishwa: 21/04/2015
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)