Wazazi wanaoingiza fitina katika manyumba yao

Swali: Ni ipi nasaha yako kwa wazazi ambao wanaingiza fitina katika manyumba yao na kwa wasichana wao kama mfano wa Intaneti na chaneli ambazo sio za kidini?

Jibu: Wamche Allaah (´Azza wa Jall). Nasaha zetu ni wamche Allaah. Wataulizwa kwa yale yaliyomo ndani ya manyumba yao na kwa wale waliyomo ikiwa ni pamoja na watoto na wanawake. Wayasafishe manyumba yao na mambo haya. Wao wenyewe wasiyaingize na wala wasimruhusu yeyote kuyaingiza katika wanawake, wavulana na watoto. Wasimruhusu yeyote kuingiza mambo kama haya katika manyumba yao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_fitan-14-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015