Jibu: Ni yapi maoni yako kwa mwenye kupinga kutokeza kwa al-Mahdiy (´alayhis-Salaam)?

Jibu: Mjinga. Huyu ni mjinga na maneno yake hayachukuliwi. Anapinga Hadiyth ambazo zimepokelewa kwa njia nyingi [Mutawaatir]. Anazipinga? Huyu ima ni mjinga au ni mpotevu. Hazingatiwi.

Kumeandikwa vitabu kuhusu kutokeza kwa al-Mahdiy na ndani yake kumebainishwa Hadiyth Swahiyh na kwamba ni lazima atokeze. Lakini watu hawa wanakadhibisha wasioyaelewa elimu yake kabla hayajawajia maelezo yake – kama Alivyosema Allaah (Ta´ala).

Mtu asiwe na papara katika mambo. Athibitishe kwanza na asimfuate mtu ni mtu na anayezungumzia mambo asiyoyafahamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_fitan-14-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015