Mwanafunzi hataki kuwafunza watu

Swali: Sisi tuna mwanafunzi alie na elimu lakini hata hivyo haitakasi elimu yake na sisi tuna haja na elimu yake atufunze. Anatumia hoja ya kwamba amebanika na kuhifadhi. Unamnasihi nini?

Jibu: Amche Allaah (´Azza wa Jall). Awafunze wajinga. Awafunze wajinga na khaswa pale ambapo watamuuliza na akawa anajua, basi katika hali hii itakuwa ni wajibu kwake kujibu:

فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

“Basi ulizeni watu wenye ukumbusho ikiwa hamjui.” (16:43)

Ni wajibu kwa mjinga kuuliza kama jinsi vilevile ni wajibu kwa mwanachuoni kujibu. Asifiche elimu:

إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَـٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّـهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ

“Hakika wale ambao wanaficha yale Tuliyoyateremsha katika hoja zilizo wazi na uongofu baada ya kuwa tumeyabainisha kwa watu ndani ya Kitabu, hao anawalaani Allaah na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani.” (02:159)

Haijuzu kuficha elimu ilihali watu ni wenye haja nayo. Elimu sio ya kwako mwenyewe bali ni ya watu wote. Ni lazima kumbainishia nayo. Hata kama hakukuuliza mbainishie. Tusemeje wakati watapokuuliza na wakakuomba nayo?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_fitan%204-13-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015