Swali: Kuna mwanamke alokuwa na mimba ya miezi saba amekufa. Wakati wa kumuosha mtoto alikuwa anafanya harakati [tumboni]. Mmoja katika waoshaji akapiga tumbo lake mpaka mtoto akaaga uhai…

Jibu: Ninajilinda kwa Allaah. Hili halijuzu. Amemuua. Lililokuwa la wajibu ni madaktari kuangalia na wakiona kuwa yuko hai wamfanyie upasuaji na kumtoa mtoto ili kumuokoa. Ama kumpiga na kumuua, ameiua nafsi – laa hawla wa laa quwwatah illa bi Allaah.

Swali: Ana nini juu yake na anapewa udhuru kwa ujinga pamoja na kujua kuwa kumeshapita miaka thelathini?

Jibu: Ujinga haukatishi haki za watu. Unaharibu mali za watu na kuua na kusema kuwa wewe ni mjinga!! Ujinga hauziangushi haki za watu. Huyu alikosea kosa kubwa. Ni lazima kwake kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) na awaombe msamaha ndugu zake mtoto huyu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_fitan2-11-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015