al-Fawzaan nasaha kwa vijana juu ya fitina za leo 1

Swali: Ni ipi nasaha yako kwa sisi vijana wenye msimamo wa Dini kutokana na fitina yenye kutokea na vipi tutatangamana na watu?

Jibu: Shikamaneni na Allaah, muombeni Allaah uthabiti na jiwekeni mbali na fitina. Jiepushe mbali na fitina na watu wa fitina kadiri na utakavyoweza. Jitenge nayo mbali. Kwa haya utasalimika nayo – kwa idhini ya Allaah.

Muhimu kuliko yote haya ni wewe kuijua. Ikiwa huijui na huitambui utatumbukia ndani yake. Jifunze fitina na aina zake. Kwa ajili hii ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akatuwekea wazi hili. Wanachuoni wametilia umuhimu Hadiyth hizi na wakawakusanyia nazo ili muweze kujiepusha nazo. Jambo la kwanza zijue. Jambo la pili jiepushe nazo na fanya sababu za kutotumbukia ndani yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_fitan2-11-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015