Dhambi kubwa haifutwi isipokuwa kwa tawbah

Swali: Je, kuna matendo yanayofuta madhambi makubwa ambayo Muislamu anatumbukia ndani yake? Mtu afanye nini akitumbukia katika madhambi haya makubwa?

Jibu: Dhambi kubwa haifutwi isipokuwa na tawbah. Dhambi kubwa haifutwi isipokuwa kwa mtu kutubia au Allaah (Jalla wa ´Alaa) Mwenyewe aisamehe. Ikiwa ni dhambi kubwa chini ya Shirki, ima Allaah Anaweza kuisamehe au yeye mwenyewe atubu kwa dhambi hiyo. Dhambi kubwa haifutwi isipokuwa kwa moja kati ya mambo mawili, ima Allaah Mwenyewe aisamehe au mtu atubie.

Kuhusu dhambi ndogo inafutiwa kwa mambo mengi. Hili lina dalili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_fitan2-11-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015