Swali: Leo fitina zimekuwa nyingi. Ni wanachuoni wepi unatunasihi kurejea kwao wakati wa fitina na majanga?

Jibu: Wanachuoni wote wa Waislamu wana kheri – Allaah akitaka. Isipokuwa tu mwanachuoni anayejuliaka kuwa na shari na balaa, huyu kusirejelewe kwake. Asli kwa wanachuoni wa Waislamu ni kuwa wana kheri na ni wenye uadilifu. Kuweni na dhana nzuri kwa wanachuoni wenu. Isipokuwa tu yule ambaye mtadhihirikiwa na kitu kutoka kwake, tangamaneni naye kwa mujibu wa kile kinachodhihirika kwake. Lakini maadamu hakujadhihirika kwake isipokuwa kheri, kuweni na dhana kwa wanachuoni wa Waislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14897
  • Imechapishwa: 21/04/2015