Waislamu leo wanauana zaidi kuliko wanavowaua maadui

Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـٰهَيْنِ مِن دُونِ اللَّـهِ

“Allaah atakaposema: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam!  Je, wewe uliwaambia watu: “Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu miwili pasi na ya Allaah?”(05:116)

`Iysaa amejibu vipi?

سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ ۚ إِن كُنتُ قُلْتُهُ فَقَدْ عَلِمْتَهُ ۚ تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ ۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ مَا قُلْتُ لَهُمْ إِلَّا مَا أَمَرْتَنِي بِهِ أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۚوَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ 

“Utakasifu ni Wako! Hainipasi mimi kusema yasiyo kuwa haki kwangu; ikiwa nimesema hayo basi kwa hakikaungeliyajua; unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yanguna wala  [mimi] sijui yale yaliyomo katika nafsi Yako; hakika Wewe ni Mjuzu zaidi wa yaliyojificha. Sijawaambia jengine isipokuwa yale uliyoniamrisha kwayo kwamba: “Mwabuduni Allaah, Mola wangu na Mola wenu, na nilikuwa juu yao shahidi wakati nilipokuwa nao. Uliponichukua juu [mbinguni] Ulikuwa Wewe ni Mwenye kuchunga juu yao na Wewe juu ya kila kitu niMwenye kushuhudia.” (05:116-117)

´Iysaa bin Maryam aliwaambia yale waliyoamrishwa na Allaah “Mwabuduni Allaah, ambaye ni Mola Wangu na Mola Wenu”. Lakini hata hivyo walikuwa wakimuabudu ´Iysaa, Maryam na Allaah. Wakisema kuwa Allaah ni mmoja katika utatu. Vipi basi itakuwa ni sahihi kwa watu hawa kujinasibisha kwa ´Iysaa na yeye anawakana mbele ya Allaah (´Azza wa Jall)?

Mayahudi, manaswara, washirikina, mabudha na wakomunisti, wote hawa ni maadui wa waislamu. Ni wajibu kwa waislamu kuwapiga vita watu hawa ili neno la Allaah liweze kuwa juu.

Lakini kwa masikitiko makubwa waislamu leo wako katika udhaifu mkubwa. Wako katika udhalilifu. Wanapigana vita wao kwa wao zaidi kuliko wanavowapiga vita maadui zao. Ndio maana maadui zao wamewasaliti. Waislamu leo tumekuwa ni kama mpira kwenye mikono ya maadui. Wanacheza vile watakavyo.

Ni wajibu kwa waislamu kukomeka na jambo hili. Wajiandae vilivyo. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّـهِ وَعَدُوَّكُمْ وَآخَرِينَ مِن دُونِهِمْ لَا تَعْلَمُونَهُمُ اللَّـهُ يَعْلَمُهُمْ

“Waandalieni nguvu zozote mziwezazo na farasi waliofungwa tayari [kwa vita] ili muwaogopeshe kwayo maadui wa Allaah na maadui zenu, na wengineo wasiokuwa wao, hamuwajui, [lakini] Allaah anawajua.” (08:60)

قَاتِلُوا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حَتَّىٰ يُعْطُوا الْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ

“Piganeni na wale wasiomwamini Allaah na wala Siku ya Mwisho, na wala hawaharamishi Aliyoyaharamisha Allaah na Mtume Wake, na wala hawafuati Dini ya haki miongoni mwa wale waliopewa Kitabu, [piganeni nao] mpaka watoe kodi kwa khiyari na hali ni madhalili.” (09:29)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/57-58)
  • Imechapishwa: 18/10/2023