Kujifunza elimu imara kwa ajili ya kupambanana Ahl-ul-Bid´ah

Ahl-ul-Bid´ah hawapigwi vita kwa silaha. Lakini hata hivyo wanapigwa vita kwa elimu na ubainifu. Ndio maana ikawa ni wajibu kwa vijana wa ulimwenguni kujifunza elimu kwa njia imara na ilio thabiti. Isiwe kwa njia ya kubabaisha kama ilivyo katika mashule mengi ambapo wanasoma elimu kwa njia ya ubabaishaji. Elimu ambayo malengo ni kutaka kupata vyeti vya masomo tu. Elimu ya kihakika ni ile ambayo inakita imara ndani ya moyo ambapo inakuwa ni kama milki ya mtu. Mtu mwenye elimu sampuli hii hajiwi na suala lolote [la kielimu] isipokuwa utaona anajua jinsi atavyolitatua kwa dalili kutoka katika Qur-aan, Sunnah na kipimo sahihi. Ni lazima mtu awe na elimu iliobobea. Watu leo wanahitaji elimu kama hii. Kwa sababu Bid´ah imeanza kusambaa katika mji wetu huu baada ya kuwa ilikuwa hakuna…

Ni lazima kupambana na Ahl-ul-Bid´ah na wanafiki kwa elimu na ubainifu. Ni lazima kubainisha ubatilifu wa yale waliyomo kwa dalili zenye kukinaisha kutoka katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maneno ya Salaf, ambao ni Maswahabah, Taabi´uun na maimamu waliokuja baada yao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/55-56)
  • Imechapishwa: 18/10/2023