Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Haya yanafahamisha kigezo cha makatazo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wanamme kujifananisha na wanawake na wanawake kujifananisha na wanamme, na kwamba msingi wa hilo hauhusiani na yale ambayo wanamme na wanawake wanajichagulia, wanayatamani na kuyachukulia ndio desturi zao. Kwa sababu mambo yangelikuwa hivo, basi ingelifaa kwa wanaume kuvaa shungi na jilbaab ambapo kusionekane kitu isipokuwa macho peke yake, na vilevile wanamme wangelipata ruhusa ya kuvaa vilemba, kofia fupi na mfano wake. Mambo kama haya yanapingana na Qur-aan, Sunnah na maafikiano. Allaah (Ta´ala) amesema kuwaambia wanawake:

وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ

”Waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao. Na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao… ”[1]

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاء الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ذَلِكَ أَدْنَى أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا

“Ee Nabii! Waambie wake zako na mabinti zako – na wanawake wa waumini – wajiteremshie Jilbaab zao; hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane wasiudhiwe. Na Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[2]

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ

“Na tulizeni majumbani mwenu na wala msijishauwe mshauwo wa wanawake majahili wa awali.”[3]

Ingelikuwa kinachopambanua mavazi ya kiume na mavazi ya kike kunatokana na yale mazowea, chaguo na matakwa yao, basi wanawake wasingeliamrishwa kujiteremshia jilbaab na shungi juu ya vifua na pia wasingeharamishiwa kujishaua kuonyesha mapambo yao kama walivyokuwa wakifanya wanawake wa mwanzo wa kipindi cha kishirikini. Kwani ndio ilikuwa ada kipindi hicho.”[4]

[1] 24:31

[2] 33:59

[3] 33:33

[4] al-Kawaakib (93/132-134) ya Ibn ´Urwah al-Hanbaliy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 151-152
  • Imechapishwa: 18/10/2023