Baadaye nikapata fatwa nzuri, yenye faida na ya kielimu ya Shyakh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) pale aliposema:

”Kofia zisizofunika nywele zote ni katika mavazi ya watoto. Mwanamke anayevaa kofia kama hizo ni mwenye kujifananisha nao. Jambo hilo mwanzoni wake zinaweza kuvaliwa na wanawake wanaokusudia kujifananisha na wavulana ambao hawajaota ndevu, kama ambavo baadhi ya wanawake makahaba hukusudia kusuka nywele zao mkia mmoja unaoning’inia katikati ya mabega yao au wakatengeneza msuko wa mikia akaiachia kwa pembeni ya mashavu na wakavaa vilemba kwa lengo la kujifananisha na wavulana ambao hawajaota ndevu. Isitoshe mwanamke muungwana anaweza kuyafanya mambo kama hayo pasi na kuyakusudia hayo, lakini bado atakuwa amejifananisha na wanamme. Zipo Hadiyth nyingi Swahiyh na nyenginezo ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wanaojifananisha na wanamme na wanamme wanaojifananisha na wanawake.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuna watu aina mbili wa Motoni sijawaona: wanaume walio na bakora kama mkia wa ng´ombe ambazo wanawapiga kwazo watu, na wanawake waliovaa vibaya, uchi, waliopinda na wanawapindisha wengine. Vichwa vyao ni kama nundu ya ngamia. Hawatoingia Peponi na wala hawatonusa harufu yake. Harufu yake inapatikana umbali wa kadhaa na kadhaa.”[1]

Wamevaa lakini bado wako uchi maana yake ni kwamba wamevaa mavazi yasiyowasitiri. Mfano wa nguo hizo ni zile nguo nyembamba ambazo zinaonyesha rangi ya ngozi yake au nguo za kubana ambazo zinazoonyesha maumbo yake, misuli yake ya nyuma, mikono ya mbele na mengineyo. Mwanamke anapaswa kuvaa mavazi yaliyopwaya na mapana ambayo hayaonyeshi mwili wake wala maunbo ya viungo vyake vya mwili.”[2]

[1] Muslim (2128) na Ahmad (2/356).

[2] al-Kawaakib (93/132-134) ya Ibn ´Urwah al-Hanbaliy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 150-151
  • Imechapishwa: 18/10/2023