52. Ni ´ibaadah zipi zilizowekwa katika Shari´ah mwaka wa 6?

Swali 52: Ni ´ibaadah zipi zilizowekwa katika Shari´ah mwaka wa sita?

Jibu: Swalah ya khofu iliwekwa katika Shari´ah wakati wa vita vya ´Asfaan katika Jumaadaa al-Uulaa.

Katika Dhul-Qa´dah Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anataka kufanya ´Umrah, lakini akazuiliwa na washirikina Hudaybiyah. Ndipo kukatolewa kiapo cha utii chini ya mti na hukumu zinazohusiana na hajj iliyokatikizwa kutokana na vikwazo vinavyokubalika kwa mujibu wa Shari´ah.

Mwaka huohuo hijjah ikafaradhishwa, ndivo alivosema ash-Shaafi´iy.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 115
  • Imechapishwa: 18/10/2023