Swali: Nimetatizwa juu ya jibu lako kuhusu kujenga kanisa. Je, kufuru inakuwa kwa kitendo chenyewe au inatokamana na I´tiqaad kwa hilo?

Jibu: Haijuzu kwa waislamu kujenga kanisa kwa sababu ni hekalu za makafiri. Hatuwasaidii makafiri. Hatuwajengei kanisa. Lakini wakikubali kuishi chini yenye hukumu ya Kiislamu na wakalipa Jizyah kuwapa Waislamu, kanisa zao zinaachwa. Lakini hata hivyo wasikarabati katika hayo. Yaachwe hayo yaliyopo tu. Kitu kikiharibika kwenye makanisa wasikitengeneze. Wasiachwe wakawa na uwezo wa kukitengeneza. Kanisa zilizopo ndio zitaachwa tu.

Ama kuhusu sisi, hatuzitengenezi, hatuzikarabati wala kuwachanga juu yake. kwa sababu kunafanywa ndani yake kufuru. Wanaamini utatu. Wanasema kuwa al-Masiyh ni mwana wa Allaah. Wanaabudu msalaba ambao wanadai kuwa uko na sura ya ´Iysaa amesulubiwa, jambo ambalo ni uongo. Hatuwaachi wakafanya hivo. hatuwajengei kanisa. Hata katika miji yao wakikubali kuishi chini ya hukumu ya Kiislamu. Hatuwaachi wakajenga kanisa mpya. Tunawaacha tu wabaki na zile ambazo zimekutwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/nawaqid-18-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/04/2015