Wanasema – Ahl-ul-Bid´ah – wanataka ukhaliyfah. Kutangaza ukhaliyfah katika nchi ya Kiislamu ni wito batili. Tuchukulie kuwa wamepata Khaliyfah ambaye anataka kuwaongoza Waislamu wote ulimwenguni. Watu tayari wameshampa kiapo cha usikivu na utiifu kiongozi Muislamu. Ni ipi hukumu ya Kishari´ah kwa yule anayekuja baada ya kiongozi Muislamu ambaye tayari watu wanamtii na kumsiliza? Hukumu ya Kishari´ah ni mtu huyo kumuua. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atapokujieni mtu na hali mmeshakuwa na uongozi kwa mtu, basi muueni huyo mtu wa pili pasina kujali ni nani.”

Hili ni kwa sababu ya kutaka kuleta umoja. Haijalishi kitu hata kama mtu huyo wa pili atakuwa ni bora kuliko mtawala aliyoko hivi sasa anayewaongoza watu.

Ama kuhusu ukhaliyfah utaotokea katika zama za mwisho utakuja itapofika wakati wake na kwa watu wanaoustahiki. Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba utakuja kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=27686
  • Imechapishwa: 11/04/2015