Swali: Je, inafaa kutaja majina ya watu wanaofanya mambo kama haya – yaani Khawaarij – juu ya minbari siku ya Ijumaa ili watu waweze kuwajua na kutahadhari nao?

Jibu: Kumtaja mtu kwa jina lake hili lina manufaa kwa watu wote. Ikiwa madhara yake ni mengi ambayo yameenea kwa vitabu vyake na mikanda yake inayoeneza Bid´ah na upotevu, watu watahadharishwe naye. Haijalishi kitu ikiwa ni juu ya minbari ya Ijumaa au katika mnasaba wowote. Watu watahadharishwe naye ili waweze kujitenga mbali na shari yake. Watu hawawezi kujitenga na shari za waovu isipokuwa mpaka wawajue. Khaswa Ahl-ul-Bid´ah hujionyesha kwa Sunnah, wema na ghera juu ya Dini ya Allaah. Hivyo inakuwa ni sababu ya kudanganyika kwa yule asiyejua hali yao. Kila yule mwenye kulingania katika Bid´ah mambo yakipelekea kuraddiwa kunafanywa hivyo. Watu hawawezi kujitenga naye mbali na yakafichuka mambo yake isipokuwa kukitahadharishwa naye. Hakika hili ni katika uongofu na mfumo wa Salaf. Hatukuwajua viongozi wa Bid´ah isipokuwa kwa wanachuoni kuandika juu yao, sawa Khawaarij, Mu´tazilah, Jahmiyyah, Murji-ah na Raafidhwah. Majina yao sio yenye kufichikana. Yanajulikana na yamesambazwa kwenye vitabu kwa sababu ya ubainifu na kutajwa sana.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=27686
  • Imechapishwa: 11/04/2015