Kwanini asikufurishwe anayehalalisha muziki?

Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kuhalalisha muziki?

Jibu: Ni kosa na ni upotevu. Lakini lau mtu huyo anazingatia tofauti juu ya suala hili na akafikiria kuwa ni dalili inayoonesha kuwa inajuzu, anapewa udhuru kwa kutofanyiwa Takfiyr. Hata hivyo ni kosa na ni upotevu kutokana na tofauti iliyopo kati ya wanachuoni. Masuala haya wanachuoni wametofautiana kwayo. Lakini usawa na haki ni kwamba muziki ni haramu. Inawezekana mtu huyo akawa anafikiria kuwa hiyo kauli nyingine ndio sahihi na hakukusudia kuhalalisha kitu ambacho ni haramu. Ni mfano wa taawili ambayo mtu anapewa udhuru kwao. Lakini hatokubaliwa kwa kauli hii. Aambiwe kuwa anapata madhambi na kitendo hichi hakijuzu. Kwa sababu kuna tofauti juu ya suala hili haina maana ya kwamba muziki unajuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/nawaqid-18-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/04/2015