Kufanya mzaha uwekaji wa mikono chini ya kitovu

Swali: Ni yapi maoni yako kwa mtu mwenye kufanyia mzaha moja ya rai ya madhehebu kama kwa mfano kuweka mikono chini ya kitovu wakati wa kuswali?

Jibu: Kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto wakati mtu amesimama katika Swalah, sawa ikiwa ataweka chini ya kitovu au chini ya kifua, ni Sunnah, na sio wajibu. Sio wajibu. Ni Sunnah.

Ikiwa anafanyia mzaha jambo lililowekwa katika Shari´ah la kuweka mkono wa kulia juu ya wa kushoto, huku ni kuritadi. Na ikiwa anafanyia mzaha tu kwa kitendo cha mtu na sio asli ya Sunnah, huu ni upotevu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/nawaqid-18-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/04/2015