Swali: Ni kweli ya kwamba hafanyiwi Takfiyr mtu mwenye kutumbukia katika moja ya mambo yanayovunja Uislamu na badala yake inatakikana kusema kuwa kitendo chake au maneno yake ndio kufuru?

Jibu: Haya ni madhehebu ya Murji-ah. Wanakabaliana na sisi kwa madhehebu ya Murji-ah? Haya ni maneno ya Murji-ah. Tunamhukumu kwa mujibu wa aloyafanya. Tunachoangalia ni ya dhahiri. Hatuna uwezo zaidi ya huo. Yule mwenye kufanya kufuru tunamfanyia Takfiyr. Yule mwenye kufanya Shirki ni mshirikina. Tunahukumu kwa yale tunayoona dhahiri. Ama mioyo hakuna anayejua yaliyomo ndani yake isipokuwa Allaah (Sunhaanahu wa Ta´ala).

Ikiwa anaomba mwingine badala ya Allaah, anaabudu makaburi na makuba na kisha akafa – je, utamuosha na kumswalia ilihali ni mshirikina? Je, utamzika katika makaburi ya Waislamu? Unachotakiwa ni kuangalia ya dhahiri na kuhukumu kwa mujibu wa ya dhahiri.

Isipokuwa tu ikiwa kama mtu ni mjinga na hajui na anaweza kuwa mjinga juu ya kitu kama hicho. Huyu anapewa udhuru kwa ujinga.

Ama kusema kuwa kitendo ndio kufuru na mwenye kitendo hicho sio kafiri? Vipi kwa mwenye kufanya kufuru asiwe ni kafiri? Vip ikwa mwenye kuzungumza maneno ya kufuru asiwe ni kafiri?

Swali: Na ili kumfanyia Takfiyr mtu kwa dhati yake ni lazima kutimie masharti kwake?

Jibu: Mtu kwa dhati yake na asokuwa mtu kwa dhati yake. Sisi tunachoangalia ni ya dhahiri. Tunawahukumu watu kutokana na yale yanayodhiri kwao. Ama kuhusu ya ndani na mioyo hakuna anayejua hilo isipokuwa Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala) tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/nawaqid-18-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/04/2015