Wafanyakazi kumpa mkurugenzi vijizawadi

Swali: Wafanyakazi wanamletea meneja wa idara peremende, biskuti na baadhi ya vyakula na baadhi ya vinywaji kama vile chai na kahawa.

Ibn Baaz: Wanamletea zawadi kutoka katika pesa zao au pesa za idara?

Muulizaji: Wanamletea zawadi kutoka katika pesa zao.

Jibu: Hapana, asichukue kitu kutoka kwao. Amefanana na kiongozi na hivyo asichukue kitu kutoka kwao. Kitendo hicho kinaweza kusababisha matatizo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22297/حكم-اهداء-الهدايا-لمدير-الادارة
  • Imechapishwa: 29/01/2023