Anza kumpa aliye kuliani hata kama ni mjinga

Swali: Mtu aanze kumuhudumia nani ikiwa katika kikao yuko mzee, mwanachuoni na ambaye amehifadhi Qur-aan?

Jibu: Aanze upande wa kulia. Akinywa basi aanze upande wa kuume. Haijalishi kitu hata kama ambaye yuko upande wa kuume ni mtu mjinga. Isipokuwa ikiwa ataomb idhini.

Swali: Aanze kumpa mtumzima au mwanachuoni?

Jibu: Aanze kumpa aliye upande wa kuume wake.

Swali: Aanze kumpa aliye upande wa kulia kwake pale tu atakapoanza kuingia katika kikao?

Jibu: Hapana. Aanze kumpa kiongozi wa kikao kisha kiongozi wa kikao ataanza kumpokeza aliye upande wake wa kuume.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22299/هل-يبدا-باليمين-ولو-كان-بالمجلس-كبير-وعالم
  • Imechapishwa: 29/01/2023