Swali: Ndugu yangu anataka kuoa binti, lakini mama yake anakataa kwa kuwa ana ndevu. Vipi anaweza kumkinaisha?
Jibu: Amuwekee wapatanishaji wazuri katika Waislamu mpaka wamweleweshe Kishari´ah ni nani anayestahiki kumuoa binti yake ikiwa kweli anampenda binti yake na hii ni katika tabia ya binaadamu kumpendea mtoto wake kheri, sawa ni wakiume au wakike. Kwa makubaliano haya ya watu wenye hekima na watoaji nasaha wazuri, atakinaika [mamake mwanamke] kuolewa na kijana huyu, mwenye ndevu, mwenye kuswali, mpwekeshaji [mtu wa Tawhiyd]. Asishtuke sana na ndevu, bali aipe kipaumbele kwanza Tawhiyd, na awe mwenye kutekeleza Shari´ah zote kama Swalah, tabia nzuri. Na katika Hadiyth:
“Atapokujieni mnayemridhia dini yake na tabia yake, basi muozesheni. Msipofanya hivyo itakuwa fitina katika ardhi na ufisadi mkubwa.”
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Imechapishwa: 19/09/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Nimemuona mchumba ananyoa ndevu usingizini
Swali: Kuna mwanaume amechumbia mwanamke. Mwanamke huyo akaona usingizini ananyoa ndevu. Akubaliane nae au hapana? Jibu: Vipi hali yake alipoamka? Swali: Alipoamka hali yake aliona kuwa ni nzuri, bi maana hakunyoa ndevu zake. Na ni mtu mzuri wa msimamo. Jibu: Mwanamke huyu aliyeona mwanaume ambaye amemchumbia usingizini kanyoa ndevu na…
In "Uchaguzi wa mke na mume"
Baba kumtafutia binti yake mwanaume mzuri
Walii kumtafutia mwanamke mwanaume mzuri ni Sunnah. 'Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu 'anh) alimuuliza 'Uthmaan bin 'Affaan (Radhiya Allaahu 'anh) kama anataka kumuoa binti yake Hafswah. Akakataa. Kisha akamuuliza Abu Bakr kama anataka kumuoa, lakini na yeye akawa amekataa. Baada ya hapo akamuomba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kumuoa.…
In "Uchaguzi wa mke na mume"
Binti analalamika kwa al-Fawzaan
Swali: Dada huyu anasema. Sisi ni kongamano la wajane. Tunataka uwashauri wasimamizi wetu miongoni mwa mababa na kaka kukimbilia kuwaozesha wasichana wao na dada zao na kutochelewesha mpaka anapokuja wa kumchumbia. Na nyinyi mnajua fika ya kwamba binti ni mwenye kuona haya kusema nataka kuozeshwa kama jinsi alivyo mvulana. Jibu: Allaah…
In "Uchaguzi wa mke na mume"