Swali: Kitu gani kinamfanya muislamu kutoka katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?

Jibu: Anatoka katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah akienda kinyume na misingi yake. Kwa mfano wale wanaowatukana Maswahabah, kuwakufurisha wenye madhambi makubwa ambayo ni chini ya shirki na akawa ni katika Khawaarij, akawa anawaua waislamu… Moja katika sifa ya Khawaarij ni kuwaua waumini na kuwaacha washirikina, kama ilivyotajwa katika Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema kuwa wanawaua waumini na kuwaacha washirikina. Ndio maana katika historia hutopata katu ya kwamba Khawaarij waliwaua makafiri; wanawaua waislamu. Kwa sababu wametoka katika madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Kadhalika Murji-ah. Wametoka katika madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, wamechukulia sahali madhambi na kuwafanyia nayo sahali watu. Wanasema kuwa imani haidhuriki na maasi. Vipi imani isidhurike na maasi? Bila ya shaka yanadhuru.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (07) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir-14340205.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015