al-Fawzaan kuhusu Takfiyr ya al-Huwayniy kwa mtenda dhambi ambaye ni mjuzi 2

Swali: Kuna wenye kusema ya kwamba mtu mwenye kuendelea kufanya madhambi makubwa anakuwa kafiri. Wenye kusema ribaa ni haramu lakini hata hivyo sintoiacha ni kafiri[1]. Ni sahihi?

Jibu: Hapana, si sahihi. Ni batili. Asiyeonelea kuwa ribaa ni halali na akataamiliana nayo kutokana na mapenzi ya pesa amefanya dhambi kubwa na kuna khatari juu yake ya kupata adhabu kali. Lakini hata hivyo sio kafiri.

[1] Abu Ishaaq al-Huwayniy amesema:

“Mtu mwenye kufanya madhambi kila siku na anajua kuwa anatenda dhambi anaonelea kuwa dhambi hiyo ni halali. Hii ni kufuru ya wazi! Mfano wa hilo ni kama yule mwenye kusema: “Mimi najua kuwa ribaa ni haramu, lakini hata hivyo nitaila. Uzinzi ni haramu, lakini hata hivyo nitafanya.” Anaonelea kuwa ni halali kabisa. Hakuna shaka yoyote juu ya kufuru ya mtu huyu!” (Mkanda “Shuruutw-ul-´Amal as-Swaalih”)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (07) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir-14340205.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015