Msimamo sahihi kwa kitabu “ar-Ruuh”

Swali: Ni yupi bora aliyeandika kuhusu roho? Je, ni sahihi kuwa kitabu cha Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) “ar-Ruuh” alikiandika mwanzoni wakati alipokuwa Suufiy[1]?

Jibu: Ndio, wanasema hivi kwa lengo la kumpa udhuru. Kitabu kina faida kubwa na kuna mambo ambayo yanahitajiwa kuangaliwa. Hata hivyo ndani yake kuna faida na maudhui kubwa. Hivi kimehakikishwa na kuchapishwa vizuri. Mtu achukue faida nzuri zilizomo humo na aache mambo yenye kutatiza. Allaah ndiye Anajau zaidi alikiandika lini. Ni sahihi ya kwamba alikuwa Suufiy. Yeye mwenyewe alikubali hilo. Amekubali kosa lake wakati aliposema:

Ee watu wangu! Ninaapa kwa Allaah, Mtukufu

Hii ni nasaha ni nasaha ya ndugu yenu alo na wasiwasi na msaidizi

Nimejaribu yote haya

na nikatumbukia kwenye wavu nilipokuwa naruka

mpaka hapo Allaah Aliponitunukia

ambaye si mkono wala ulimi wangu hauwezi kumfidia

mwanachuoni kutoka Harraan

Allaah Amjaze kheri kweli kweli

kwa Pepo na radhi

Alinishika mkono na kwenda na mimi

mpaka akanionyesha inapotoka imani

Yeye mwenyewe amekubali hilo kwenye “an-Nuuniyyah”. Mwanzoni alikuwa na Taswawwuf na maoni yanayohitajiwa kuangaliwa. Wakati alipokutana na kigogo huyu Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah akanufaika naye, akajifunza haki na akapata elimu ya kubobea na ukaguzi. Allaah Amrahamu.

[1] Tazama al-Fawzaan kuhusu kitabu cha Ibn-ul-Qayyim “ar-Ruuh” – al-Firqah an-Naajiyah (firqatunnajia.com)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (07) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir-14340205.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015